Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Mashariki yalianza mwaka 1993 chini ya kilichokuwa Chama cha Wakulima Tanzania yaani “Tanzania Agricultural Society Organization” kwa kifupi TASO. Hata hivyo, kutokana na sababu za kiutendaji na kimaadili za TASO, kuanzia Mwaka 2017, Serikali ilitoa Mamlaka ya Usimamizi wa Uwanja kwa Sekretarieti za Mikoa ya Kanda ya Mashariki inayojumuisha Mikoa minne (4) ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani na Tanga.
Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki kuwa kitovu cha ujuzi/teknolojia ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ujasiriamali nchini
Kuwawezesha wakulima, wafugaji, wavuvi na wajasiriamali kufikia adhma yao kwa kuimarisha ushirikiano katika uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya maendeleo ya uwanja; kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma; kuruhusu mawazo mbadala na ubunifu; kuongeza na kudhibiti vyanzo vya mapato; kuimarisha ulinzi na usalama na kuboresha utoaji huduma