Kamati Kuu


Ndiyo Kamati ya Maamuzi ya utekelezaji wa mipango na majukumu yote ya Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki. Mwenyekiti wa Kamati hii ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Katibu wake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro. Wajumbe wa Kamati hii ni Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji/Manispaa/Miji/Majiji kutoka Kanda ya Mashariki na wataalamu wa sekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Maliasilii, Afya, Miundombinu, biashara n.k. Majukumu ya Kamati hii ni kupitia Taarifa za maandalizi kutoka Kamati ya Wataalam na kufanya maamuzi ya mwisho kuhusu shughuli za Maonesho.