Meneja wa Uwanja
Ofisi ya Meneja wa uwanja imeanzishwa ili kutatua changamoto ya ukosefu wa mwendelezo wa utekelezaji wa mipango na majukumu ya Maonesho ya Nane Nane mara baada ya maonesho kumalizika. Hali hii imesababisha uwanja wa maonesho kuwa “dormant” kutokana na kukosa msimamizi na hivyo kuzorotesha ufanisi wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki. Meneja wa Uwanja ana majukumu makuu mawili; utekelezaji na ufuatiliaji wa maazimio ya Kamati Kuu na uratibu wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya uwanja kwa mwaka mzima.