Kamati ya Uratibu


Kamati hii huratibu shughuli zote za maonesho zikiwemo; Kuandaa vikao vya maandalizi; kuandaa ratiba za viongozi; kuandaa mapokezi ya viongozi; kuandaa hotuba za wageni; kuandaa na kusambaza barua za mialiko; Kusimamia na kuratibu utendaji wa Kamati zote; kuandaa taarifa ya maonesho; kuandaa gari la matangazo na kutoa matangazo.  Mwenyekiti wa Kamati hii ni Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Morogoro huku Makamu wake akiwa Mkurugenzi wa Kampasi ya LITA Morogoro. Wajumbe wa Kamati hii ni Mshauri wa Kilimo (RAA) Mkoa wa Morogoro; Afisa Mifugo Mkoa wa Dar es Salaam; Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na Tanga; Mshauri wa Kilimo Mkoa wa Tanga, Dar es Salaam na Pwani na Afisa Mifugo Mikoa ya Morogoro, Pwani na Tanga.