KATIBU TAWALA AMEWATAKA WAFANYABIASHARA WA UNGO WANAKUZA SOKO LA BIDHAA HIYO

Katibu Tawala wilayani ulanga Bw Iman Mlyapatali amewataka watengenezaji wa nyungo kuhakikisha wanakuza soko la nyungo kwa kuzisambaza maeneo mbalimbali ndani nan je ya wilaya ya ulanga Amezungumza haya alipofika kwenye banda la ulanga kkwenye maonesho ya nane nane yanayoendelea katika viwanja vya nane nane mjini Morogoro ambayo yanayobeba kanda ya mashariki Amesema kuwa nyungo zinazotoka ulanga zimeoneka kuwa bora hivyo amewataka wanaoshughulika na nyungo hizo kuongeza soko la nyungo ili watanzania wafaidike na nyungo zianzotoka ulanga ‘Nyungo zetu ni nzuri sana kwa hiyo niwashauri muongeze soko la nyungo kwani wilaya yetu imebarikiwa kuwa na nyungo bora hivyo mtafute masoko sio mahnge tu bali hata ifakara nma maeneo mengine ya nje ya ulanga amesema mlyapatali” Mbali bna hilo katibu Tawala huyo amepita na kuona bidhaa mbalimbali zinazotoka Ulanga na kupongeza juhudi kubwa za wakulima waliopo kwenye banda la maonesho la ulanga kwa kazi nzuri wanayofanya ikiwemo kulima na kufuga kisasa

Posted in matangazo, Tangazo on Aug 07, 2023