Kamati za Usimamizi wa shughuli za Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki


Jumla ya kamati Saba (7) zinaunda Kamati za Maonesho. Kamati hizo zimefafanuliwa hapa chini:

i. Kamati ya Maonesho

Kamati hii huandaa na kuratibu vigezo vya mashindano, huandaa vikombe na vyeti kwa washindi pamoja na kuprint Tshirt, Stickers, vitambulisho na mabango ya matangazo. Wajumbe wa Kamati hii ni; katibu Tawala sehemu ya uchumi na uzalishaji  Tanga; Mshauri wa Kilimo Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanasheria Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa Morogoro, Mshauri wa Kilimo Mkoa wa  Morogoro na Afisa Ushirika Mkoa wa Morogoro.


ii. Kamati ya Chakula

Kamati hii huratibu zoezi la upatikanaji wa chakula kwa msafara wa wageni rasmi wakati wa Maonesho. Pia huandaa chakula wakati wa vikao vya maandalizi, siku ya ufunguzi na siku ya kufunga. Wajumbe wa Kamati hii ni Mkuu wa Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji (AAS- E) Morogoro, Mkuu wa Sehemu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu (AAS-SS) Morogoro, Mshauri wa Kilimo (RAA) Mkoa wa Tanga, Afisa Mifugo Mkoa wa Morogoro na Afisa Mifugo Mkoa wa Dar Es Salaam


iii. Kamati ya Mapato na Matumizi

Kamati hii huratibu shughuli zote zinazohusiana na ukusanyaji na matumizi ya mapato. Majukumu ya kamati hii ni pamoja na; kuainisha vyanzo vya mapato; kusimamia ukusanyaji wa mapato; kuandaa bajeti ya mapato na Matumizi, kusimamia matumizi kwa mujibu kwa bajeti, kuandaa taarifa ya mapato na matumizi na kuandaa matokeo ya matumizi.

Wajumbe wa Kamati hii ni Mhasibu mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Morogoro, Afisa Mifugo Mkoa wa Pwani, Mshauri wa Kilimo Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Sehemu ya Manunuzi Mkoa wa Morogoro na Afisa Mifugo Mkoa wa Dar Es Salaam.


iv. Kamati ya Mapambo na Burudani

Kamati hii huhusika na majukumu yafuatayo; kupamba jukwaa (mahema, viti podium na meza) siku ya ufunguzi na siku ya kilele; kutafuta na kumsimamia mshereheshaji; kuandaa vikundi vya burudani; kuandaa mabango na kuyasimamisha na; kuandaa matarumbeta siku ya kufungua na siku ya kilele. Wajumbe wa Kamati hii ni Afisa Kilimo Mkoa wa Morogoro; Afisa Uvuvi Mkoa wa Morogoro, Afisa Kilimo Mkoa wa Pwani na Afisa Mifugo Mkoa wa Pwani.


v. Kamati ya Miundombinu, Usafi na Afya

Kamati hii huhusika na majukumu yafuatayo: Ufuatiliaji wa ukarabati wa barabara; Usafi wa mazingira  wakati wa Maonesho; Ufuatiliaji wa ukarabati wa mageiti na majengo na kufuatilia miundombinu ya umeme. Wajumbe wa Kamati hii pamoja na; Afisa Mazingira wa Mkoa – Morogoro; Afisa Afya wa Mkoa wa Morogoro; Afisa afya wa Manispaa Morogoro; Mhandis ujenzi wa Manispaa Morogoro na Afisa Biashara Mkoa.


vi. Kamati ya Ulinzi na Usalama

Kamati hii hutekeleza majukumu yafuatayo; kuimairisha ulinzi uwanjani; kudhibiti wafanya biashara wanaokiuka taratibu; kudhibiti washiriki ambao hawasajili ushiriki wao; Kusimamia ulinzi katika milango ya kuingilia; Kudhibiti njia haramu za kuingia ndani ya uwanja. Wajumbe wa kamati hii ni Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya; Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Pwani; Afisa Mazingira Mkoa wa Morogoro, Afisa Kilimo Mkoa Morogoro na Katibu Tawala Wilaya ya Morogoro.


vii. Kamati ya Habari na Mawasiliano

Kamati hii huratibu shughuli zote za uandaaji na usambazaji wa habari na makala za habari. Wajumbe wa Kamati hii Afisa Habari wa Mkoa wa Morogoro, Mwandishi wa Habari (TBC), Mwandishi wa Habari (Star TV), Mwandishi wa Habari (Abood Media), Mwandishi wa Habari (Moro PC), Mwandishi wa Habari (TNS), Mwandishi wa Habari (Iman Media).