DED ULANGA AWAKARIBISHA WANANCHI WOTE KWENYE MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya ulanga Ndg Saida Mahugu amesema wilaya ya ulanga imebarikiwa kulima mazao ya biashara na mazo ya chakula hivyo amewakaribisha wadau wa kilimo kufika banda la Halmashauri ya ulanga ili kujifunza kilimo zaidi

Bi Mahugu amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la halmashauri ya wilaya ulanga kwenye maonesho ya nane nane yanayofanyika mjini morogoro

Mahugu amesema kuwa kuna kanda mbili ambazo zimekuwa zinafanya vizuri kwenye kilimo ikiwemo kanda ya mwaya yenyewe inajihusisha zaidi na kilimo cha bishara kwa kulima mazao kama pamba,korosho cocoa na mazao mengine ya biashara,huku ukanda wa lupiro wenyewe unalima mazao ya chakula kama mpunga,mahndi na mazao mengine ya chakula

“Ulanga tuna kanda mbili za kilimo kwani ukanda wa mwaya unajihusisha sana na kilomo cha biashara kama pamba,korosho, ufuta na mazao mengine,lakini kwa ukanda wa Lupiro wenyewe ni mahususi kwa kilimo cha chakula kama vile mpunga”

Aidha Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema kuwa mapato makubwa yanayopatikana kwenye halmashauri yake yanatokana na kilimo hivyo amewataka wakulima wilayani kwake kuendelea kulima kisasa na kijifunza zaidi kwa wakulima wengine kwenye maoneso hayo ya nane nane

Posted in matangazo, Tangazo on Aug 07, 2023