Dira, Dhamira na Misingi Mikuu
Dira:
Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki kuwa kitovu cha ujuzi/teknolojia ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ujasiriamali nchini
Dhamira:
Kuwawezesha wakulima, wafugaji, wavuvi na wajasiriamali kufikia adhma yao kwa kuimarisha ushirikiano katika uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya maendeleo ya uwanja; kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma; kuruhusu mawazo mbadala na ubunifu; kuongeza na kudhibiti vyanzo vya mapato; kuimarisha ulinzi na usalama na kuboresha utoaji huduma
Maadili/Misingi Mikuu:
Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki yanazingatia msingi mikuu minane (6) ambayo ni:
- Ushirikishwaji wa wadau
- Ubunifu na Uthubutu
- Utendaji kazi uliotukuka
- Uwajibikaji wa pamoja na uwazi
- Haki na Usawa na;
- Mwiko wa kutoa wala kupokea rushwa