DC KILINDI AWASHAURI WAKULIMA NA WAFUGAJI KUWEKEZA KATIKA UFUGAJI WA SAMAKI

Mkuu wa wilaya Kilindi Mh:Hashim Mgandilwai amewataka wafugaji wa samaki wilayani Kilindi kuanza ufugaji wa Kambare ambao wanafaida kwa wafugaji Alitoa wito huo jana wakati alipotembelea banda la maonesho ya Nanenane la Halmashauri ya Wilaya Kilindi na kuzungumza na wakulima,wafugaji,wajasiriamali na wataalam kutoka Wilaya Kilindi Alisema samaki Kambare wanaweza kufugwa na kuleta faida kwa kuwandaalia mazingira ya mabwawa yanayoendana na mahitaji ya samaki hao Alisema wataalam wa mifugo katika Halmashauri ya Wilaya Kilindi watoe elimu kwa wafugaji samaki ili waanze kufuga Kambare Akizungumzia kuhusu bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wa Halmashauri ya Wilaya Kilindi Mh:Mgandilwa alisema wataalam washirikiane na wajasiriamali kutafuta soko la bidhaa zao pamoja na kuwashauri kubuni logo/nembo , brand/chapa na vifungashio vyenye mvuto wa kibiashara ili kukuza soko la bidhaa zao Sanjari na hilo Mh:Mgandilwa alisema umefika wakati sasa kwa wakulima wilayani Kilindi kuanza kilimo cha ndizi aina ya mkono wa Tembo ambazo zina soko na zinapendwa na walaji Alisema ndizi za mkono wa Tembo huwa sio nyingi kama ndizi nyingine lakini huwa ni kubwa na bei yake sokoni ni nzuri.

kaulimbiu ya maonesha haya 2023 "VIJANA NA WANAWAKE NI MSINGI IMARA WA MIFUMO ENDELEVU YA CHAKULA"

Na Modi Mngumi Kitengo cha mawasiliano Kilindi dc

Posted in matangazo, Tangazo on Aug 04, 2023