FAHAMU ZAO LA MNANAA “MINTI”

Minti ni zao la kibiashara na mara nyingi limekuwa likitumika kama kiungo ambacho kinaweza kutumika kwa kuweka kwenye chai au chakula lakini pia limekuwa likutumika kwenye utengenezaji wa dawa za meno.

Zao hili linapandwa kwa mfumo wa vipandikizi na baada ya kupandwa unavuna baada ya miezi mitatu na utaendelea na umwagiliaji wa maji na uwekaji wa mbolea ili yaweze kuota majani mengine.

Minti ni moja kati ya mazao yanayouzwa kwa gharama kubwa sokoni na ni hadimu kupatikana.

Ukizingatia sheria na taratibu za kilimo ukipanda minti kwenye shamba la hekta moja utaweza kupata tani 20 na kwa maeneo yenye Hali ya hewa ya joto ni vizuri kupanda kwenye eneo la kivuli mfano katikati ya migomba.

Tembelea Banda la Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwenye viwanja vya J. K Nyerere hapa Mkoani Morogoro maonesho ya nanenane upate fursa ya kujifunza bure masuala ya kilimo, mifugo na uvuvi hutojuta kutembelea banda hilo.

Posted in matangazo, Tangazo on Aug 03, 2023