WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO LA KILINDI

Waziri wa maliasili na utalii Mh:Mohamed Mchengerwa atembelea banda la maonesho ya nanenane la Halmashauri ya wilaya Kilindi na kushauri vijana na watanzania kwa ujumla kuacha shoka na wakamte mazingira ili kuongeza uzalishaji wa asali kwa lengo la kuongeza pato la kaya na taifa

Alisema ufugaji nyuki unaenda sanjari na utunzaji wa mazingira na vitendo vinavyofaanywa na jamii kuharibu mazingira kwa kukata miti hovyo vinatishia uharibifu wa mazingira na makazi ya wadudu hao wenye faida kubwa katika kuongeza pato la nchi

Alisema uzalishaji asali unaweza kuongeza pato la taifa kutoka dola milioni 15 kwa sasa hadi dola milioni 100 ifikapo mwaka 2025 na kuwataka watendaji katika ofisi yake kuacha kukaa ofisini na badala yake waende vijijini kutoa elimu kwa wafugaji Nyuki na kuwashauri kutenegeneza mizinga ya kuvutia nyuki wadogo

Mh:Mchengerwa alisema ongezeko hilo la fedha za kigeni kupitia uzalishaji wa Asali linawezekana kwa sababu fedha za kuwaelimisha na kuwawezesha vijana,wanawake na wazalishaji wa Asali zipo na serikali imeijpanga kuhakikisha lengo la kuongeza uzalishaji Asali linafanikiwa.

kaulimbiu ya maonesha haya 2023 "VIJANA NA WANAWAKE NI MSINGI IMARA WA MIFUMO ENDELEVU YA CHAKULA"

Na Modi Mngumi Kitengo cha mawasiliano Kilindi dc

Posted in matangazo, Tangazo on Aug 05, 2023