IJUE TOFAUTI KATI YA GREEN HOUSE NA SCREEN HOUSE

Kitalu nyumba “green house” ni aina ya kilimo kinachofanyika ndani kwa kujengewa na kuwekewa mifumo ya kudhibiti hali ya hewa tofauti na ilivyo kwa Kitalu nyumba aina ya “screen house” na kilimo cha nje “open field” ambacho ni ngumu kwa mkulima kuweza kudhibiti hali ya hewa hasa Hali ya joto.

Hayo yamesemwa na Ndg. Pascal Stephano Moswery ambae ni Mtaalamu wa Kilimo biashara akiwa kwenye maonesho ya nanenane ndani ya Banda la Manispaa ya Ubungo viwanja vya J.K Nyerere vilivyopo Mkoani Morogoro.

Moswery ameendelea kueleza kuwa Green House ni kilimo kinacholipa zaidi ukilinganisha na kilimo cha screen house au open field kutokana na uwepo wa Mitambo inayotumiwa kwenye kilimo hicho ya kudhibiti hali ya hewa na hivyo kupelekea Mkulima kupata mazao mengi na yenye ubora wa hali ya juu.

Aidha, Moswery ameendelea kueleza kuwa mara nyingi kilimo cha green house au screen house huwa kilimo kinachofanyika kwenye eneo dogo hivyo ni vyema mkulima kuchagua mazao yenye kulipa zaidi ambayo atayauza kwa gharama kubwa mfano letusi, hoho za rangi, matango, nyanya na mengineyo ya aina hiyo.

“Kumbuka kuwa kulima sio suala la kuweka mbegu au kupanda tu mche na kumwagia maji Mkulima ni lazima kuzingatia sheria na taratibu za kilimo ili uweze kupata mazao mengi na yenye ubora” Alisema Moswery

Ikumbikwe kuwa miongoni mwa faida za kufanya kilimo cha green house au screen house ni kuzuia wadudu ambao wengeweza kuingia kwenye mazao na kutagaribu.

Moswery amepanda mazao mbalimbali kwa kutumia kilimo cha screen house ndani ya eneo lililopo kwenye bando la Manispaa ya ubungo zikiwemo hoho za rangi “colured cupscum” letusi nyekundu na kijani, nyanya, pilipili zizisowasha “paprika” pamoja na matango “british cucumber” ambazo zimestawi vizuri na kwa ubora.

Tembelea Banda Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwenye viwanja vya J. K Nyerere hapa Mkoani Morogoro kwenye maonesho ya nanenane upate fursa ya kujifunza bure masuala ya kilimo, mifugo na uvuvi hutojuta kutembelea Banda hilo.

Posted in matangazo, Tangazo on Aug 03, 2023